Sunday, January 17, 2016

Tangazo

Uongozi wa Skuli wa Biasha Mombassa - Zanzibar, unawapongeza wanafunzi wote waliobahatika kujiunga na na skuli hio na pia waliobahatika kujiunga na skuli nyengine kwa kucahaguliwa kuendealea na masomo yao kwa ngazi ya O-level (kidato FI-FIV , kwa mwaka 2016). 
Pia tunachukua fursa hii kuwakaribisha katika katika skuli yetu hii kwa mara ya kwanza. Hivyo tunawaomba wawe wamefika kwa wakati wakiwa na vifaa vyote kwa ajili ya kuanza masomo yao rasmi.
Vile vile kwa mara nyengine tunachukua nafasi hii kunawapongeza wale wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tatu (FIII) katika skuli tofauti za Unguja na Pemba, tunawambia hapa ndo kazi imeanza, wawache mchezo na wapige Kazi Tu!..

Tuseme tu "KARIBUNI SANA"

N.B:
"Our Motto is to provide a quality education in such that it can be benefited to the Learners"

Friday, January 1, 2016

Tangazo

Uongozi wa Skuli ya Biashara (ZCSS) - Zanzibar, inawatangazia wanafunzi wote kuwa, Skuli itafunguliwa siku ya Jumatatu sawa na January 04, 2016.
Wanafunzi wote wanatakiwa wawe wamefika skulini saa 12:45 asubuhi. Vile vile wanatakiwa kutayarisha ada ya Skuli ili kuweza kulipa kwa wakati, kwa sababu hakuna kinachoweza kutekelezwa (kama huduma na mengineyo) bila mchango wa ada.

Tangazo hili limetolewa kwa kuzingatia matakwa ya uongozi wa Skuli (ZCSS).

Ahsanteni...!

N.B:
"Our Motto is to provide a quality education in such that it can be benefited to the Learners"